Skyner Ampa Makavu Nay wa Mitego
Msanii  wa hip hop, Nay wa mitego amechezea kichambo kutoka kwa mzazi mwenzake  ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Skyner Ally kuwa ameshindwa kuwa  baba bora kwa binti yake.
Kwenye  ukurasa wake wa instagram Skyner amefunguka maneno hayo akiwa anamtakia  heri ya kuzaliwa mtoto wake ambaye amefikisha miaka mitano na kudai  kuwa alikuwa na dukuduku kutoka moyoni ndani ya miaka mitano na baada ya  kuongea tayari limetoka.
"Thats  face you make when you see your 'daddy jina' anakufanyia promotions na  kudanganya watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi  unayovaa hajui thamani yake maskini. nimevumilia sana It's 5 Years now  nimejiskia kutapika na nimetapikaa.  Am done Mungu wa mbinguni nakuomba  unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki..... uzima wa afya  nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa  nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake" aliandika Skyner.
Aidha skyner ameendelea kufunguka kuwa "Endelea  na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki...Please unapost  picha za mtoto wangu za nini...shobo dundo zanini? Sitaki shobo na  mwanangu koma kama ulivyo komaaa...Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda  watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa  nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi  Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done"- Aliongeza Skyner.
Skyner hakuishia hapo  aliendelea kutoa usia kwa binti yake kwa kuonyesha jinsi alivyo na umuhimu katika maisha ya binti yake "Hakuna  anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba'ko hana  analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha  kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie  nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki  nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama  bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy  Birthday My Happiness"- Skyner alimaza 
Maneno  hayo makali kwa Skyner yalikuja muda mfupi baada ya Nay kuweka picha ya  binti yake na kumtakia heri ya kuzaliwa na kudai kuwa amenunua bastola  kwa ajili ya kumlinda.

No comments