Kauli ya Jerry Muro baada ya Haji Manara wa Simba kufungiwa na TFF
Muda  mfupi  baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya  nidhamu ya TFF kutangaza kumfungia mkuu wa idara ya habari na  mawasiliano wa Simba Haji Manara kwa utovu wa nidhamu na kukutwa na  makosa matatu.
Afisa habari wa zamani wa Yanga ambaye nae alifungiwa mwaka mmoja Jerry Muro ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika “Mtuache  sasa tupumzike, tuliyofanya kwa taifa hilo haswa kwenye mpira nadhani  yametosha, Waswahiba karibu kijiweni @hajismanara“
Mkuu  wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara amefungiwa mwaka  mmoja kujihusisha na soka pamoja na faini ya Tsh Milioni 9.
Kamati  ya nidhamu ya TFF imetoa adhabu hiyo licha ya Haji Manara kushindwa  kufika kwa madai ya kupata dharura lakini anayo nafasi ya kukata rufaa.

No comments