Msemaji wa Simba afungiwa kujihusisha na soka kwa mwaka mmoja
Kamati  ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia Haji Manara  (Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba)  kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia anatakiwa kulipa  faini ya Shilingi  Milioni tisa.
Makamu  Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa amesema hatua hiyo  imefikiwa baada ya Manara kukutwa na makosa matatu dhidi ya TFF ambao ni  walalamikaji.
Makosa  hayo ya Manara dhidi ya mlalamikaji TFF ni kuituhumu na kuidhalilisha  TFF, kueneza chuki za ukabila na la tatu kuingilia utendaji wa  shirikisho hilo.
Siku chache zilizopita  Manara aliituhumu TFF kufanya njama za waziwazi ili kuwabeba wapinzani wao Yanga kwenye Ligi Kuu.
Manara  pia aliwatuhumu viongozi wakuu wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake,  Selestine Mwesigwa ni wahaya na viongozi wa zamani wa Yanga, ambao  wanataka kuipendelea Kagera Sugar.

No comments