Samia Suluhu: Kero za Muungano zitatatuliwa kwa mazunguzo ya pande Mbili
Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan  amewahimiza wananchi kudumisha na kuuenzi Muungano wa Taganyika na  Zanzibar na kuwahakikishia wananchi wa pande Mbili kuwa kero chache za  Muungano ambazo zimebaki zitamalizwa kwa mazungumzo kama hatua ya  kudumisha Muungano huo.
Makamu  wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti  katika Mahojiano na vyombo Mbalimbali vya habari katika kuelekea katika  Kilele cha Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo  sherehe za kitaifa mwaka huu kwa mara ya Kwanza zitafanyika kwenye  Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Makamu  wa Rais amesisitiza kuwa tangu Muungano huo uasisiwe umekuwa na manufaa  makubwa kwa pande zote Mbili kwani jamii zimefahamiani na kushirikiano  vizuri katika shughuli za kiuchumi na za kimaendeleo hasa uimarishaji wa  ulinzi na usalama kwa wananchi wa pande Mbili.
Aidha,Amesema  hatua zinazochukuliwa za kutatua kero za Muungano kwa haraka ni jambo  jema na la msingi kwani linalenga kuhakikisha Muungano ambao umefikisha  miaka 53 sasa unakuwa ni Muungano wa mfano wa kuigwa Duniani.
Kuhusu  elimu ya Muungano wa Vijana, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan  amesema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi za Kiserikali za pande Mbili  kuweka mikakati mizuri ya kuelemisha vijana wa sasa kujua umuhimu wa  Muungano ili waweze kuuelewa na kuudumisha.
Amesema  kwa sasa vijana wengi wanafuatilia sana mitandao ya kijamii hivyo ni  muhimu kwa taasisi za kiserikali zinazoshughulia Muungano kuweka  utaratibu wa kupeleka ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano kwa jamii hasa  vijana kwa ajili ya kuwaelimisha faida za Muungano.
Makamu  wa Rais pia amehimiza makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi  wastaafu nchini waendelee na jitihada zao katika kuelimisha umma ili  kuuelewa vizuri Muungano kwa ajili ya faida ya jamii nzima na ya Taifa  kwa ujumla.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
DODOMA.
25-April-2017

No comments