Mtatiro: CUF haina walinzi wa chama wenye bastola
Mwenyekiti  wa Kamati ya Uongozi, The Civic United Front (CUF) Julius Mtatiro  amefunguka na kusema chama cha CUF hakina walinzi wa chama wenye bastola  wala hakina walinzi wanaozunguka mitaani kufanya doria.
Julius  Mtatiro ametoa ufafanuzi huo leo baada ya Mkurugenzi wa Habari CUF  Taifa, ambaye anamuunga mkono Profes Ibrahim Lipumba  ndugu Abdul  Kambaya kukiri kuwa ni kweli wao walituma vijana kwenda kwenye Kata ya  Mabibo kufanya doria. 
"Siku  ambapo kikao kinafanyika Vinna Hotel, vijana wetu pia walikuwa kwenye  doria, tulipozungumza na vyombo vya habari tulikiri na tunaendelea  kukiri hatuna sababu ya kukataa kwamba tulituma vijana wetu na  walikwenda kwenye doria" alisema Kambaya 
Kufuatia  taarifa hiyo ya Kambaya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, The Civic  United Front (CUF) Julius Mtatiro amefunguka na kusema wao kama CUF  hawana walinzi wa chama wenye bastola hivyo amelitaka jeshi la polisi  limtumie huyu Kambaya kueleza kijana aliyekuwa na bastola yuko wapi na  walikodishwa kutoka wapi.
"Leo  amekiri kuwa lile Zombi lililopigwa na wananchi, Mabibo, eti lilitumwa  na genge la Mungiki/Lipumba ili kufanya doria kwenye kata ya Mabibo.  Yani eti Lipumba ana jeshi lake linalofanya doria na kupiga watu  mitaani. Sasa Polisi wasitafute mchawi, huyu Abdul Kambaya aeleze lile  zombi lililokuwa na bastola liko wapi na waliikodisha kutoka wapi?  Alihoji Mtatiro 
Mbali na hilo Mtatiro alizidi kusisitiza kuwa wao hawana walinzi wa chama 
"Halafu,  eti huyo msemaji wa Lipumba anasema "Zombi" hilo lililokamatwa ni  "mlinzi wa chama". Napenda ifahamike kuwa CUF haina walinzi wa chama  wenye bastola, na pia hakuna chama cha siasa chenye walinzi wanaozunguka  mitaani kufanya doria, wameajiriwa na serikali ipi? Alihoji Mtatiro 

No comments