Askofu Gwajima Kununua Treni ya Umeme
Mchungaji  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amedhamiria  kununu treni ya umeme baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya  kujenga reli ya kisasa(standard gauge).
Amesema  kuwa treni hiyo itatumika siku za ibada kubeba waumini huku wakiimba  nyimbo za kumtukuza Mungu. Lakini pia alisema atakuwa tayari kuruhusu  itumike kubeba abiria wa kawaida.
Askofu  Gwajima aliyasema hayo jana kanisani kwake, ambapo alieleza gharama za  treni hiyo ni TZS bilioni 11 lakini hakusema ni lini hasa atainunua.
“Siku  moja nilimchukua mwalimu Bihagaze, alikuwa mwalimu wangu wa Biblia,  nikamwambia twende nikakuonyeshe mji wa mwanakondoo, nikamchukua na  helkopta hadi shambani ambapo ni mji utakuwa na mahoteli, universities,  kituo cha mafuta na kila kitu,”  alisema.
Alifafanua kuwa katika mji huo, kuna ramani inaonyesha kuwa reli inapita katikati. “Alipopaona  akasema mbona kuna reli inapita katikati, nikamwambia nitanunua treni,  akashangaa akaniuliza, treni ni shilingi ngapi? Nikamwambia dola milioni  nne na mabehewa yake dola milioni tano hivi, akasema nikulipie?  Nikamwambia nitanunua mwenyewe. Akapiga magoti kusujudu nikamwambia yapo  mengi yanakuja,” alisema Askofu Gwajima huku waumini wake wakimshangilia kwa shangwe.
Ujenzi  wa reli uliozinduliwa na Rais Dkt Magufuli Aprili 12 mwaka huu,  utakamilika ndani ya miezi 30, ambapo kwa awamu ya kwanza utaanzia Dar  es Salaam hadi Morogoro, treni ikiwa na uwezo wa kukimbia umbali wa  160km/hr. Treni itakuwa na jumla ya mabehewa 100.

No comments